Wednesday, February 4, 2015
On Wednesday, February 04, 2015 by Mtumishi wa mungu na mkewe, samson mboya
VIPENGELE9VYA MAOMBI
Na Mtu wa Mungu Nabii Samson Mboya,
SOMO
VIPENGELE 9
VYA MAOMBI
Utangulizi:
Maisha ya mwanadamu Muongozo mzima wa kuishi kwetu tunaupata
kutoka katika kitabu kitakatifu yaani Bibilia Takatifu maombi ya watu wengi
hayajibiwi kwakuwa hayana kanuni maombi yanakanuni na misngi,kanuni
nivileunavyoelewa Neno kwa undani,msingi ni Neno lenyewe,Yesu akawafundisha
wanafunzi wake kuomba Mathayo 6:9, sala hii niamtukuza Mungu imebeba
msamaha,chakula cha kila siku na mahitaji yote, ila kuna Zaidi ya hayo hebu
tuangalie maandiko Zaidi,
YOHANA 14:14-31 14:13-31. Katika mistari hii, pamoja na mambo mengine,
tutajifunza kuhusu, Namna ya kuomba“.
(1) KUOMBA KWA JINA LA
YESU (MST. 13-14)
Yesu Kristo aliye Bwana na Mwalimu wetu, hapa anatufundisha
jinsi ya kuomba, ili maombi yetu yawe na uwezo wa kipkee wa kuleta majibu
kutoka kwa Mungu. Anatuelekeza kumwomba
Mungu baba, kwa JINA LA YESU, na anarudia maelekezo haya tena na tena (YOHANA
16:23-24). Shetani, adui yetu, hataki
tuombe kama tulivyo elekezwa kuomba , hivyo mbinu yake kubwa, ni kutufanya
tuombe kinyume na maelekezo ya Yesu.
1.1 Muovu
anafahamu Nguvu iliyo katika Jina la Yesu
Hataki tuombe kwa usahihi anataka tuwaombe watakatifu Petro,
Yohana, Yakoba, n.k. Watuombee. Yote haya, ni kinyume na maelekezo haya ya
Yesu. Maelekezo ya Yesu kwetu ni “Nanyi
Mkiomba“,. Wanaotajwa kutuombea katika
Biblia, ni wawili tu hapa Roho Mtakatifu na Yesu mwenyewe; (MATENDO 1:13-15). Kutumia sanamu za watakatifu fulani katika
maombi yetu, hivyo ni kinyume na
maelekezo haya. Mungu ni Roho, inatupasa
kumwabudu KATIKA ROHO NA KWELI, na kuikimbia ibada ya sanamu, maana sanamu au
Kuabudu mizimu,hizi ni dhambi mbele za Mungu Hii ni pamoja na kushiriki kupiga
ramli, n.k (ISAYA 31:7; ZABURI 135:15-18; 1 WAKORINTHO 10:14).
(2)
HAKIKA YA
KUJIBIWA MAOMBI (MST. 13-14)
Yesu Kristo hapa anatuelezea juu ya hakika ya kujibiwa
maombi. Anasema, tukiomba kama
alivyotuelekeza kwa Jina la Yesu, hilo tunaloliomba, atalifanya. Hata hivyo, hatuna budi kuviondoa vikwazo
vingine vya kujibiwa maombi, vinavyotajwa katika maandiko, ili hakika ya
kujibiwa maombi itende kazi kwetu.
Hatuna budi kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu au Neno lake (1 YOHANA
5:14-15; MATHAYO 20:20-23). Hatuna budi
pasipo kutaka kuvitumia kwa tamaa zetu (YAKOBO 4:3). Hatuna budi kuomba pia kuwa mbali na dhambi
au uasi wa sheria za Mungu (MITHALI 28:9; 15:29; YAKOBO 4:2-7), na pia hatuna
budi kuomba kwa imani, pasipo shaka yoyote (YAKOBO 1:6-7). Tukiondoa vikwazo hivi, hatuna budi kuwa na
hakika ya kujibiwa maombi kwa wakati wa Mungu uliokubalika.
(3) ALAMA YA KUMPENDA
YESU (MST. 15, 21, 23-24)
Wako watu wengi ambao wanassema wanampenda Yesu, hata hivyo,
wengi kati yao wanapenda kwa neno tu, siyo kwa tendo na kweli (1 YOHANA
3:18). Yesu anatufundisha alama
itakayoonyesha kwa tendo na kweli kwamba tunampenda Yesu. Alama hii, ni kuzishika amri zake zote,
kulishika neno lake na kulitendea kazi kama lilivyo, bila kulijadili. Yeyote anayesema anampenda Yesu huku
hayashiki maneno yake, huyu ni mwongo. Na lazima ufahamu kama wewe ni mwongo
ujuwe unamtumikia shetani maana maandiko yanatufundisha wazi, kila atendaye
dhambi ni wa ibilisi na ibilisi ni Baba wa uwongo, ili kuomba unahitaji
kusaidiwa,
(4) Msaidizi wa maombi
yetu (MST. 16-17, 25-26)
Yesu Kristo alipokuwa duniani, alikuwa Msaidizi wa kipekee
kwa wanafunzi wake. Hata sasa
anatusaidia sisi (2 WAKORINTHO 6:2; WAEBRANIA 2:18; 13:6). Kabla ya kuondoka, anatutambulisha kwa
Msaidizi mwingine. Msaidi huyu, siyo
Mtume Mohamed, kama wengine wanavyodai.
Msiaidizi huyu, ni ROHO WA KWELI, siyo mtu. Ulimwengu hauwezi kumpokea, wala kumwona kwa
macho, wala kumtambua; naye atakuwa NDANI ya wanafunzi wa Yesu, naye anakaa nao
MILELE (MST. 16-17). Sifa hizi zote,
haziko kwa mtume yeyote mwanadamu.
Wengine wote hawakuwa ndani ya watu na pia hawakukaa milele! Msaidizi huyu wingine ni ROHO MTAKATIFU (MST.
25-26). Huyu hutusaidia udhaifu wetu wa
kuomba (WARUMI 8:26), na kutufundisha na kutukumbusha yote, na kutuongoza
atutie kwenye kweli yote. Msaidizi huyu,
ni wa muhimu mno kwetu ikiwa tunataka kuwa mashahidi wa Yesu (MATENDO
1:8). Pasipo Msaidizi huyu, hatuwezi
kuwaleta watu kwa Yesu kwa mfanikio makubwa (YOHANA 16:7-8).
(5) SITAWAACHA NINYI
YATIMA (MST. 18-20)
Yesu hakutuacha yatima.
Siyo tu ametuachia Msaidizi mwingine, lakini tukiwa wawili watatu
tumekusanyika kwa jina lake, yupo kati yetu katika roho (MATHAYO 18:20). Kwa sasa tunamwona katika roho, hata hivyo
atakuja kwetu wakati wa kunyakuliwa kwa kansia na tutamwona katika utukufu wake
akiwa ndani ya Baba.
(6)
FAIDA
ZA KUZISHIKA AMRI ZA YESU (MST. 21-23)
Tukizishika amri za yesu, Baba na Mwana wote hutupenda. Yesu akitupenda hivi, anajidhihirisha kwetu;
kutuonyesha upendo wake katika kututendea mengi, katika roho na mwili. Tukizishika amri za Yesu, Baba na Mwana, hufanya
makao kwetu. Wakifanya makao kwetu,
hatutapungukiwa kitu, wala hatuna haja tena ya kuogopa lolote.
(7) MSIWE NA WOGA (MST.
27-29)
Woga, ni kinyume na imani (MARKO 4:40). Woga hautokani na Mungu, bali Shetani (2
TIMOTHEO 1:7). Tukiruhusu woga au hofu
kututawala, tunampa Ibilisi nafasi ya kutupa adhabu (WAEFESO 4:27; 1 YOHANA 4:18). Ikiwa baba, Mwana, wamefanya makao kwetu, na
roho Mtakatifu pia yuko ndani yetu, na ni Msaidizi wetu, kwa nini tuogope kama
kwamba tuko wenyewe? Yesu kwa kutupa
maelezo haya, anazidi kusema “Amani yangu nawapa“, Amani nawaachieni“. Amani yake Yesu aliyotupa, itafuta kila namna
ya hofu ndani yetu. Kama tuna hofu,
tupokee amani hii ndani mwetu, kwa imani.
(8) MKUU WA ULIMWENGU HUU HANA KITU KWA YESU (MST.
30)
Mkuu wa Ulimwengu huu yaani watu wa ulimwengu huu wenye
dhambi, ni Ibilisi au Shetani (1 YOHANA 5:19; WAEFESO 2:1-2; WAKOLOSAI
1:13). Yesu hapa, anatuhakikishia kwamba
Shetani hana kitu chochote kwake.
Tunapoomba na kuliitia Jina la Yesu, hatuna haja ya kuogopa, Shetani
hana kitu kwa Bwana wetu Yesu! Majini
yote hayana kitu kwake. Hatuna haja ya
kuogopa vitisho vya mapepo tukiwa na Yesu!
(9) JINSI YA KUUJULISHA
ULIMWENGU YA KUWA TUNAMPENDA BABA (MST.
Hapa, Yesu anatuonyesha jinsi ya kuujulisha ulimwengu ya
kuwa tunampenda Baba. “Kama Baba alivyomwamuru, ndivyo afanyavyo“, ni
kielelezo cha Yesu kwetu. Je, kama baba
anavyotuamuru katika neno lake, ndivyo tufanyavyo? Kama sivyo, hatumpendi..
************************************************************************
Je Unataka kuingia mbinguni?
Ni utakatifu tu siyo cheo cha kanisa flani wala siyo ujuzi elimu ya
mtu(WAEBRANIA 12:14). Ndani yake
hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi. Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la!
Maisha yako yamejaa
dhambi, pamoja na kusema wewe ni Mkristo na kanisani unakwenda sadaka na
mafungu ya kumi unatoa bado; wewe pia ni
mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha
kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia
mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA
14:6). Je, uko tayari kutubu sasa ili
upate rehema hii? Tafuta Mchungaji akusaidie kukupa muongozo wa sala ya toba
Ikiwa unahitaji msaada Zaidi wa ushauri na maombezi
Usisite kuwasiliana na Mtu
wa Mungu Nabii Samson Mboya
Piga simu 0756 809 209 huduma hii ni bure,
Search
Popular Posts
-
Na Mtu wa Mungu Nabii Samson Somo : KUHARIBU MADHABAHU YA ADUI JUU YA MAISHA YAKO Utangulizi Kimsingi kufanikiwa au kuharib...
-
Maombi ya kupinga Roho ya mauti, 2Wafalme 4:40 Utangulizi: Roho ya mauti unaweza kuipinga kwa maombi isaya 38:1 ...
-
VIPENGELE 9 V YA MAOMBI Na Mtu wa Mungu Nabii Samson Mboya, SOMO VIPENGELE 9 VYA MAOMBI Utangulizi: Maisha...
-
Kuuoshwa miguu Yohana 13:3-8 Utangulizi Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitok...
-
Ujimbe watu waliyowekewa mipaka ya kutofanikiwa Utangulizi Kuna watu wengi Sana hatima zao zimewekewa mipaka na hiyo ndiyosababu k...
-
MAUTI YA KUTOSAMEHE Warumi 6: 23 Utangulizi: Watu wengi wamekufa kiroho au kimwili kwasababu ya kutokusamehe na kuachilia wengine ...
Recent Posts
Blog Archive
Powered by Blogger.