KARIBU SANA RAFIKI YETU MUNGU ANATAKA KUKUSAIDIA KAMA UKOTAYARI KUPOKEA MSAADA WAKE KUPITIA SEHEMU HII UNANAYOISOMA SASA HIVI ZAIDI YA MASOMO PIA UNARUHUSIWA KUPIGA SIMU KWA MSAADA WA USHAURI NA MAOMBEZI HUDUMA HII NI BURE KWA MTU YEYOTE, 0756 809 209 ITAPOKELEWA NA YULE MTU WA MUNGU NABII SAMSON MBOYA

Blogger news

Thursday, September 29, 2016

On Thursday, September 29, 2016 by Mtumishi wa mungu na mkewe, samson mboya



Ujimbe watu waliyowekewa mipaka ya kutofanikiwa


Utangulizi


Kuna watu wengi Sana hatima zao zimewekewa mipaka na hiyo ndiyosababu kubwa maisha yao kuwa vile yalivyo leo unaweza kujiwekea mipaka wewe mwenyewe kwa tabia yako bila kujuwa, wazazi kwakukulaani,watu waliokuzungukaau kwakulogwa,kukosa ufahamu wa kiMungu


zao maarifa imeandikwa Daniel 2; 20 hata katika kuteseka imeandikwa Hosea 4;6


Tofauti nyingine ya mtu na Mtu ni Matumizi ya akili zake juu ya kile anachokitaka, kufanya, kusema, kuona, kusikia,


Kuna watu akili zao zimewekewa mipaka  na mapepo  kiasi kwamba wanafikiria wamefika mwisho,wakuishi,kufanikiwa,kusoma,biashara,kazi, kuoa au kuolewa kumbe bado mwisho  ule mpaka ndiyo unaomtesa kuendelea na safari,


Mstari wa kukumbuka Daniel 2; 20


Mpaka ni kizuwizi kinacho zuwia kati ya pande mbili ili jambo la upande mmoja lisiende upande mwingine


AINA ZA MIPAKA ANAYOWEZA KUWEKEWA MTU


Mpaka ni makubaliano baina ya pande mbili juu ya uhuru wa jambo flani, mpaka wa kwanza ni wa kiroho,na wakimwili


Mpaka unaweza kuwa wa maneno,au maandishi,au kitu ila kiuhalisia mpaka unaanzia rohoni na  unaishia rohoni kwa alama za mwilini,


  • Kuna watu akili imewekewa mipaka ya kufikiria
  • Kuna watu wamewekewa mipaka kwa kulaaniwa
  • Kunawatu akili waliyowekewa mipaka kwa vitisho
  • Kunawatu akili  wamewekewa mipaka kwa zawadi flani
  • Kunawatu akili wamewekewa mipaka kwa ahadi nyingi nzuri anabaki kusubiri uzee unamkuta bado anasubiri
  • Kuna watu akili wamewekewa mipaka kwa kutishiwa na jamii, eneo, mazingira.
  • Kunawatu akili wamewekewa mipaka ya magonywa ya mapepo
  • Kunawatu akili wamewekewa mipaka ya kibri cha mapepo
  • Kunawatu akili wamewekewa mipaka ya ujinga wa kimapepo
  • Kunawatu akili wamewekewa mipaka ya roho za mizimu
  • Kunawatu akili  wamewekewa mipaka kwa kulogwa
  • Kunawatu akili wamewekewa mipaka ili wao wafanikiwe kichawi
  • Kuna watu akili wamewekewa mipaka ya stress,


 


Sasa kuna kifungo ambacho unaweza kumwona mtu yuko vizuri lakini akili yake imefungwa. Sasa kwanini mungu ametupa akili ni kwasababu kuna mambo mengine tunaweza kuyafanya kwa akili tu Unaweza kumshuhudia mtu anakwambia jambo flani hadi ukamshangazwa kumbe akili imewekewa mpaka na mapepo  ndio maana mungu alivyowaumba watu akaweka mambo mengine tusimsumbue ila tutumie akili zetu.


MFANO: Maisha tunayoishi Mungu aliyawekea utaratibu namna ya kuishi kujilinda na uovu,kuishi kwa kumtii Mungu, kuisikia sauti ya Mungu Kumb 28:1 Unahitaji Baraka za wapi shambani,mjini,kazini,familia


AKILI YA DARASANI NA YA MTAANI INAHITAJI UTOFAUTI KIDOGO


Akili ya masomo na akili ya mtaani


Mtu anaweza kusoma vizuri sana akija kwenye upande wa kutunza familia akaanza darasa jipya na baadhi ya mitihani asipokuwa makini akapata sifuri, watu wanabaki kusema mbona amesoma sana?uvumilivu wa masomo na uvumilivu wa ndoa nitofauti kidogo  Akili inaweza kuwekewa mipaka na mapepo, kama umewahi kusikia watu wakisema amekamatwa masikio


Imeandikwa “enyi waume ishini na wake zenu kwa akili” unakuta mtu anaakili ya bihashara kutunza familia yake anashindwa, anaakili ya kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa,hata eneo lake la kazi anaongoza mamia ya watu kazini ila mke  au mme mmoja anamshinda kunasehemu kunampaka anahitaji msaada, wa ushauri na maombi


 


Hii ndiyo sababu ninashawishika kukushauri wewe kumpokea Yesu awe bwana na muokozi wa maisha yako ili kupata ufahamu Mpya ili kila kitu kiwe kipya   kilichozaliwa na roho ni roho,


Imeandikwa Mithali 3:19 kwa hekima bwana aliiweka misingi ya nchi; kwa akili zake akazifanya mbingu imara;


Kuna watu wakianza kufikiria mambo ya maana wanaumwa akili na wengine wanahela mkonononi lakini hawajui jinsi ya kizitumia na kuna watu wanatumia akili za watu kufikiria na kufanya maamuzi na wengine wameibiwa akili zao hawawezi kufanya mambo ya maendeleo yake anatajirisha wengine, kila kukicha mwisho akili yake inarudi arithini


 Hii ndiyo sababu makaburini kunakuwa na dhamani kubwa sababu watu wanalala na akili ikiwa haijatumika kabisa na hakuna mtu wakuja kuzitumia wengine wanajipa moyo mtoto wangu atakuwa jembe, kama wewe ulikuwa ndiye mzazi ukawa mpini mtoto atatoa wapi uwezo wa kuwa jembe na umemjengea msingi gani wa yeye kuwa vile unavyofikiria wewe nayeye kuna Hatari ya kuzikwa na akili zake zote, Imeandikwa Hosea 4:6.


Unapokataliwa na Mungu unageuka mali ya ibilishi utaanza kuishi maisha mapya ya utumwa na mateso waibilisi (wachawi) wanaweza kuloga akili ya Mtu, akashindwa kufikia malengo,


Imeandikwa Wagalatia 3:1-enyi wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao yesu kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?


Imeandikwa Kutoka 7:11 ndipo farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa misri wakafanya vivyo kwa uganga wao.


Wenye akili wanauwezo kuliko wachawi na waganga, akili ya kumwambia mtu jambo akalifahamu na kukubaliana nalo hiyo ni akili ya mtu.


Akili iliyohuru ni ya dhamani sana,


Maisha mazuri unayoyataka hutakiwi kumuuliza Mungu Unachotakiwa ni kutumia akili kama haijawekewa mipaka Mungu ni wautaratibu usipopata ufahamu unaweza kukaa unassubiri Mungu waka Mungu nay eye anakusubiri wewe,


 Biblia inasema mtu akizaliwa akaishi miaka mia asipate chakula kizuri na asiishi vizuri ni afadhali mimba iliyoharibika.


Kutoka 35:35 amewajaza watu hao akili za moyoni, ili watumike katika kazi kila aina, ya mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu, na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yo yote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.


Mungu alikuwa anamwambia musa katikati yako nimewaweka watu wenye akili wanaoweza kufanya mambo makubwa.


Kumbukumbu ya torati 1:15


15 basi nikatwaa vichwa vya kabila zenu wenye akili, waliojulikana, nikawafanya wawe vichwa juu yenu, maakida ya elfu elfu, na maakida ya mia mia, na maakida ya hamsini hamsini, na maakida ya kumi kumi, na wenye amri, kwa kadiri ya kabila zenu.


Kama akili imefungwa unaweza ukaenda kaburini na akili ikiwa bikra.


DALILI ZA AKILI ILIYOWEKEWE MIPAKA


1 mambo ya nyakati12:32


35. na wa wana wa isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.


Akili ya mtu inaweza kuwekewa mpaka ili isifikirie maendeleo anayoyataka


1.       Akili yako inapanga mipango ambayo wewe hutaki na hujawahi kuwaza kuifanya, mipango inayopangwa kule kwenye akili yako inakujia na wewe umekaa na hujawahi kufanya hiyo unayoiwaza si rahisi  


2.akili iliyo wekewa mipaka  apoanza kupanga mipango ya maendeleo kichwa kinauma,au kuchanganyikiwa  na anashindwa kuendelea kufikiria au hasira inamtawala kabisa bila sababu,


3. Akiawaza jambo litakalompa mafanikio mazuri gafla anahisi uwoga,wa kushindwa,


4. Anaanzisha miradi mingi kwa garama kubwa utekelezaji ni hakuna


5. Unaota kila mara ndoto za mafanikio ila zinabaki katika mawazo mazuri na simulizi


6. Unakuwa na shahuku ya kufanya jambo flani au kuwa kama flani ila hofu inakufunika mwisho unakuwa msimulizi


7. Kila unalolianzisha au kujaribu unajilinganisha na mtu flani ndugu au jamaa wa karibu aliyeshindwa


8. Ukifanya jambo likikaribia kufanikiwa basi linakuja wazo la matumizi makubwa au uharibifu flani amba hata wewe hujatarajia,


Shule inaongeza maarifa akilini ila kutumia maarifa uliyonayo kufanya kile unachokitaka ni habari nyingine mtu kukaa pale alipo na kuridhika ni moja ya mpaka,


Mfano mwanzilishi wa kampuni ya simu za apple mr stivi kama angekufa kabla hajatoa simu ya apple ungeenda kule kaburi ya inchi yake ungeona simu zote za apple zimelala kaburini kama una macho ya rohoni. Sio kiwango cha elimu kinakutambulisha wewe bali ni kiwango cha akili ile utakayoitumia ndiyo itakutambulisha na watu kusema anaakili sana mtu huyu


 Inawezekana akili yako inatumiwa sehemu flani na wewe hunufaiki hata kidogo ushauri wangu unahitaji maombi ya kurudisha wizi huo wa akili yako,


Yeyote anayeimarisha utawala ufalme wake Kwa kutumia akili yangu ninawateka nyara kwanzia sasa maana imeandikwa Yeremia 30:16


Hata Kama wameibiwa akawekewa mipaka panahitajika maombi maalumu ya kupanua mipaka yao wawe huru Isaya 42:22 watu walioibiwa na kutekwa’ ninaamuru akili iliyoibiwa irudi Kwa jina la yesu kristo kwa damu ya yesu. Katika jina la yesu nabomoa ngome inayozuia akili kwa damu ya yesu. Naondoa wigo uliowekwa kwenye akili yangu kwa jina la yesu, naondoa wigo wa hofu, naondoa wingi wa mashaka kwa damu ya yesu.


Lazima kubomoa ukuta waliowekewa kwamba wasiolewe,wasifanye biashara inchi za njie,wasiolewe au kuoa,wasisome sana,wasipate nafasi ya uongozi,wasikubalike katika jamii, wasiishi maisha yao halisi,wasiwe walikotakiwa kuwa,


Katika jina la Yesu,