KARIBU SANA RAFIKI YETU MUNGU ANATAKA KUKUSAIDIA KAMA UKOTAYARI KUPOKEA MSAADA WAKE KUPITIA SEHEMU HII UNANAYOISOMA SASA HIVI ZAIDI YA MASOMO PIA UNARUHUSIWA KUPIGA SIMU KWA MSAADA WA USHAURI NA MAOMBEZI HUDUMA HII NI BURE KWA MTU YEYOTE, 0756 809 209 ITAPOKELEWA NA YULE MTU WA MUNGU NABII SAMSON MBOYA

Blogger news

Thursday, September 29, 2016

On Thursday, September 29, 2016 by Mtumishi wa mungu na mkewe, samson mboya

Maombi ya kupinga Roho ya mauti,



2Wafalme 4:40

Utangulizi:      Roho ya mauti unaweza kuipinga kwa maombi isaya 38:1

Mauti inaweza kujificha sehemu ya aina yeyote ile maana ni roho isiyoonekana kirahisi inaweza kuuwa kiumbe, kitu, au jambo flani, husika, lililolengwa kuuwawa, ambavyo inahitaji macho ya rohoni kuiona na kuiondoa, pia kunahitajika nguvu za Rohoni,

 Mauti ni Nguvu ya Uharibifu, inayoweza kuingia katika kiumbe, kitu, au mazingira wakati wowote kwa yeyote kwa chochote kwaajili ya kuuwa, ndiyo maana inaitwa jina la mauti,

Mara nyingi mauti inaanzia roho japo matokeo ni mwili, baada ya kuona viashiria ndipo utasikia vilio leo Mungu anataka kukusaidia

Roho ya mauti inaweza kumtesa mtu kwaajili ya,

Mfano:

  • Ufahamu kutokuwa na taarifa sahihi inaweza kukusababishia kifo
  • Roho ambayo hainaulizi wa roho wa bwana,
  • Jamii iliyokuzunguka yaani washauri wakiwa hawana ufahamu matokeo
  • Mazingira yaliyokuzunguka yanaweza kukusababishia mauti
  • Tabia inaweza kuruhusu mauti ndani yako
  • Kukosa nguvu ya kiroho ndani yako,(Elisha alikuwa rohoni,

 

   Isaya 42:2 watu wanaweza kuibiwa wao au roho zao kupitia uchawi Kuna majini au majoka ambayo yanaingia ndani ya mwili wa mtu na kuitoa roho yake. Haya ukipeleka hospitali si rahisi kuona katika vipimo vyao Hospitali wanaweza kupima macho, punzi, na mzunguko wa damu,mfumo wa hewa,viungo mfumo wa akili, kama vinafanya kazi na kama havifanyi  kazi jibu wanasema kiungo kimekufa au mtu mwenyewe.

Watu waliyoiona mauti ndani ya sufuria,
“Basi wakawapakulia hao watu ili wale. Ikawa, walipokuwa katika kula chakula, wakapiga kelele, wakasema, Mauti imo sufuriani, Ee mtu wa Mungu Wala hawakuweza kula.” 2Wafalme 4:40


Maombi ya elsha kupinga roho ya mauti
Kama mauti ipo ndani ya sufuria basi kumbe mauti inaweza kuwa  ndani ya gari yako,mauti inaweza kuwepo ndani ya nyumba yako,mauti inaweza kuwa ndani ndoa,shamba lako,Biashara yako, inaweza kuingia katika Huduma yako ikafa, inaweza pia kuagizwa popote kwa yeyote wakati wowote, kifo ni uharibifu,au ni utengano na kinaweza kumtenga mtu na familia yake,

Kinaweza kutenganisha ndoa, kinaweza kumtenga mtu na kazi yake.  Kinaweza kumfuata mtu kikamuingia na kumtenganisha na mwili wake au kumtenganisha na jambo lolote alilo nalo.
 Dalili ya Mtu mwenye roho ya mauti,

  • Anaandamwa na majanga  kila namna yasiyoeleweka chanzo nini
  • Kila analoanzisha hata kama ni zuri kiasi gani lazima life au liishie njiani
  • Ni mtu wa kufanya maamuzi ya haraka na baadayekujutia maamuzi yake
  • Ni mtu wakupuuzia kila jambo analoshauriwa,
  • Ni mtu mwenyekiburi kikubwa sana
  • Ni mtu wa kujitenga tenga na wenzake
  • NI mtu wa kushambuliwa na magonjwa yasiyoeleweka
  • Ni mtu wa kuandamwa na ajali zinazoandamana kwa msimu flani
  • Ni mtu asiyekuwa na makazi ni wa kuhama hama ovyo,
  • Ni mtu anayedhufika na wakati mwingine haumwi
  • Ni mtu mwenye hasira isiyonakiasi,

Waliyowahi kuona roho ya Mauti,

“Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi. Imeandikwa Ufunuo wa Yohana 6:810

kwa kuwa kifo ni roho Basi roho chafu zinaweza kutumia mauti kukumaliza mapepo, majoka, mizimu, majini na miungu. Kifo hakina macho lakini hakikosei kifo hakina kichwa ila kina kina akili kinaweza kujua kule kilikotumwa na kujuwa kunanaendeka au hakuendeki mauti inaweza kuishi na Mtu kwa muda mrefu kabisa isipoondolewa basi inamaliza kazi,

Maombi ya Hezekia kupinga roho ya mauti

Imeandikwa,Isaya 38:1-7 Hezekia  tayari mauti ilisha ingia ndani na chanzo kilisha patikana ilikuwa inangoja muda wa kumaliza kazi ya kumuuwa ezekia,

Kwa mfano anayejifika mabomu, tunasema mauti ndani ya mtu,anayetoa mimba,anayepiga mke,au mme,anayetumia madawa ya kulevya,anayechokoza wengine,anayedhulumu pesa ya mwenzake,anayezini na mke asiye mke wake,anayefanya uasherati,anayeiba,chochote cha mtu,iwe pesa au mke,

Kifo kinaweza kuwekwa kwenye gari.kikaishi Kwa muda kusubiri chanzo au sababisho ili kuuwa.

Kuna mapepo  yanayoweza kuitwa na wachawi, na kuagizwa kuleta mauti katika maisha ya mtu aliyekusudiwa  niliwahi kufundisha alama za mapepo  maringo,kupita kawaida , ukahaba, kuharibu mimba, kuvunja ndoa, kusababisha utasa,ajali zisizoeleweka vyanzo na mambo mengine. Kuna majini/mapepo ya uchizi, kuna mashetani maalum yanayotenda kazi kulingana na ngazi zao na maagizo. Mapepo yanayosumbuwa Huduma ni tofauti na la biashara,

Si kila maombi yanajibiwa kirahisi tu,
“Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.” Imeandikwa Daniel 10:13

Kuna majini ya aina Fulani ambayo yanatumwa kwenda kumwingia mtu na kukaa ndani yake kusubiri tarehe iliyopangwa ili kutenda kazi iliyokusudiwa.

Kifo kilikuwa ndani ya sufuria kinangoja watu wale chakula ili wafe,

Kifo kilikuwa ndani ya sufuria kinasubiri watu wale lakini kikateguliwa na Mtu wa Mungu Elsha hii inadhihirisha kuwa watu wengi wanatembea na kifo ndani yao bila ya wao kujua. Unaweza kuona kwamba mtu anaona hatari iko mbele yake lakini anaenda bila kuiona kwasababu kifo kiko ndani yake kimempofusha macho asiione na kinasubiri nafasi ili kimtenganishe na mwili wake.

Kila unayemwona hapa duniani anatumikia utawala wa juu au wa chini kwa kujua au bila ya yeye kujua.

Inawezekana rafiki yako wa kazini anakuonea wivu jinsi unavyofanikiwa akakuendea kwa mganga wa kienyeji ili ufe umuachie nafasi uliyo nayo. Akifika anapewa masharti na Yule mganga anatuma kifo kuja kwako. Kifo kinaweza kutumwa kwa mtu kulingana na mazingira aliyo nayo.

Mapepo hayapendi kutambuliwa kujulikana hutengeneza mazingira ambayo watu wakiangalia watasema marehemu alifariki kwa ajali, kwa kuugua, kwa presha na watu wakiangalia wanakubaliana na hali hiyo kumbe ni kifo kimemchukua mtu huyo.

Roho ya mtu inaweza kutolewa na joka au jini ambalo linakuja kuingia ndani ya mtu kuitoa roho ya mtu. Kwasababu roho ndiyo imtiayo mwili uzima kwahiyo roho ya mtu ikitolewa nje ya mwili, mtu huyo unaacha kufanya kazi. Mtu huyo anaitwa amekufa, marehemu
 

Mauti ikiwa mahali jina linabadilika kwa mtu anaitwa maiti,au marehem ndani ya mji utaitwa Mji wa mauti unaitwa mji wa mauti kwa sababu kazi yake kubwa ni kusababisha mauti.

2WAFALME 2:19 “watu wa mjini wakamwambia Elisha, angalia twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri kama bwana wangu aonavyo, lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapoza”. Unaweza ukawa unafanya biashara Fulani na unaweza ukawa unapata faida lakini kumbe ndani ya biashara hiyo kuna mauti. Kwa mfano: biashara ya bodaboda, watu wanasema “asante mchina ametusaidia” lakini angalia jinsi ambavyo watu wengi wanakufa kutokana na hizo bodaboda. Katika ndoa watu wanajifunguwa wanakufa ovyo, mitaa mingine uwezi kusikia harusi hata siku moja utasikia taarifa za msiba tu, kuna mtaa kila biashara inayoanzishwa lazima ife maana mauti ipo ndani ya mtaa,

 

Pata maarifa leo na uanze mapambano

“Kwa mamlaka ya jina la Yesu kila roho ya mwanadamu, mashetani, kifo, na mapepo yote na miungu yote ya mauti  kokote kwa yeyote palipowekwa roho ya mauti iliyotumwa kuja kuingia ndani yangu, kwenye biashara yangu, kwenye kazi yangu,uchumba,ndoa,mashamba, ili nife zife,au kazi yangu ife ninaondoa kwa jina la Yesu, ninazifunga na kuzivunja roho zote zilizotumwa kwangu kwa mamlaka ya jina la Yesu. Amen”

wakala wa kerubi anaweza kutuma roho ya mauti ikakutesa hadi kifo,

 Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu;

je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe? Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo. Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege.” Ezekiel 13:1820