KARIBU SANA RAFIKI YETU MUNGU ANATAKA KUKUSAIDIA KAMA UKOTAYARI KUPOKEA MSAADA WAKE KUPITIA SEHEMU HII UNANAYOISOMA SASA HIVI ZAIDI YA MASOMO PIA UNARUHUSIWA KUPIGA SIMU KWA MSAADA WA USHAURI NA MAOMBEZI HUDUMA HII NI BURE KWA MTU YEYOTE, 0756 809 209 ITAPOKELEWA NA YULE MTU WA MUNGU NABII SAMSON MBOYA

Blogger news

Thursday, September 29, 2016

On Thursday, September 29, 2016 by Mtumishi wa mungu na mkewe, samson mboya

MAUTI YA KUTOSAMEHE
Warumi 6:23
Utangulizi:
Watu wengi wamekufa kiroho au kimwili kwasababu ya kutokusamehe na kuachilia wengine wameua hatima zao,vipaji,biashara,uchumba,ndoa,kazi Huduma,kuhubiriuchungaji, watu kwa kutokuweza kusamehe wamezika maisha yao bila kufahamu huu ni ufahamu, usijeukawa miongoni mwao,
Ki uhalisia mwanadamu anapoishi mahalipamoja mtu Zaidi ya Mmoja lazima kuwe na mitazamo tofauti, huruka tufauti katika hali hiyo ndio inazaa tofauti wa kutokukubaliana kunasababisha sura mpya inayoitwa  kwazo kwa pande moja au kote,
Makwazo yanapokuwapo upendo unaondoka chuki inastawi ambayo inakaribisha roho ya kisasi hiyo ikimwingia mtu anafanya analolitaka kwa mwingine,na hapo ndipo hasara inaingia ya yule anayesababisha kisasi, ndiyo maana ya ujumbe tunaojifunza leo mauti ya kutosamehe,
kukoseana kupo maana nikutokubaliana au kutokuelewana lakini hakutufanyi kulipizana  kisasi bali kunatakia kutufanya kusamehana, tunajifunza somo hili mwisho utaweza kusamehe walewanaokukosea, usemi wangu
  • Usipende kusamehewa penda kusamehe
  • Usipende kupendwa penda kupenda
  • Usipende kupewa penda kutoa
  • Usipende kutendewa jema penda kutenda jema
  • Maana kila anayetenda anapanda mbegu,atakayoivuna
Madhara 12 ya kutokusamehe,
Nini maana ya kusamehe(mauti)
Maana ya kusamehe ni kuachilia na kusahau na Hatusamehe kwa sababu ya faida ya waliyotukosea  bali tunasamehe kwasababu yetu sisi wenyewe,
maana msamaha ni kwaajili ya yule anayesamehe si kwaajili ya anayesamehewa, inawezekana umeshutuka kidogo kwamba inakuwaje nikosewe mimi alafu nisamehe kwa faida yangu, nataka kuombwa msamaha
usiposamehe-utaumia,
Usilipize Kisasi Hata ikiwa umefanyiwa ubaya wa namna gani, Biblia inafundisha na inakusihi usilipize kisasi kwa huyo aliyekufanyia ubaya. Imeandikwa,
"Wapenzi, msijilipizie kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, kisasi ni juu yangu Mimi, Mimi nitalipa, anena Bwana" (Warumi 12:19)

Sababu zinazosababisha mtu kulipiza kisasi,
Sababu kuu ya mtu kulipiza kisasi kunasababishwa na kutokusamehe na kusahau anapokosewa moyo unazaa sumu ya kuuwa kila siku,
1. Kutokusamehe na kuachilia kunakusababisha kuishi katika dhambi wakati wote unapoishi hapa duniani kitu kinachoweza kukunyima uzima wa milele, ni dhambi,(dhambi ni mauti)imeandikwa warumi 6:23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
2. Kutokusamehe na kusahau kunakusababishia kuwa mbali na Mungu hofu ya mungu ikikosekana unajikuta unafanya dhambi
3. Kutokusamehe na kusahau  kunakunyima haki yako ya umwana mbele za Mungu,na mbele ya jamii iliyokuzunguka
Kutokusamehe na kusahau kunaweza kukusababishia ugonjwa usiyo na dawa,
5. Kutokusamehe na kusahau kunamzuwia Mungu kukusamehe wewe unapo omba msamaha mbele zake, Mathayo 6:12 Utusamehe makosa yetu, kama sisi nasi tulivyokwisha kuwasamehe waliyokwisha tukosea.
6. Kutokusamehe na kusahau kunamzuwia Mungu kuwa upande wako imeandikwa warumi 8:31
7. Kutokusamehe na kusahau kunasababisha mapigo kwako mwenyewe ,Mungu atakuwa adui wa adui zako
Kutokusamehe kunasababisha kulipiza kisasi, ukifanya hivyo umepanda mbego ambayo mwisho utavuna  uharibifu au mauti
7. kutokusamehe kunazalisha mauti ya Huduma,uchuma,ndoa,biashara,kazi,mashamba nk
8. Kutokusamehe na kusahau kunakufanya upate asara usizotarajia katika maisha yako aibu kwa maamuzi utakayoyafanya
9. kutokusamehe kunakupotezea watu wa muhimu katika maisha yako,au kuhama maeneo
10. kutokusamehe kunachelewasha maendeleo kama ni uchuma inabidi msubiriane kwa muda mrefu sana, na mwingine anaweza kuoa au kuolewa
11. kutokusamehe kunasababisha uvamizi wa mapepo machafu,
12. Kutokusamehe kunakusababishia upate aibu isiyotarajiwa,inayoweza kukusababisha ulipize kisasi ambacho na kisasi utapojaribu kulipiza tu hasara inaingi,
Dawa ya kosa siyo kulipiza ni kusamehe,
Nyeyote unayemlipizia kisasi iwe ndugu, marafiki, wanandoa, wachumba, kazini, wakulima, wafanyabiashara, wachungaji, kuna asara kubwa Sana, pia mbingu huwa inamcheka mtu wa namna hiyo,
Kwanza unapopanga au nuwia kulipa kisasi kwa ndugu yako au rafiki kwa mtu yeyote Mungu anakucheka,
 Zaburi 37:12 -16 Asiye haki hunuia mabaya juu ya mwenye haki, Na kumsagia meno yake.
Bwana atamcheka, Maana ameona kwamba siku yake inakuja.
"Wapenzi, msijilipizie kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, kisasi ni juu yangu Mimi, Mimi nitalipa, anena Bwana" (Warumi 12:19)

Kuna hasara zinazoweza kukupata ukiamua kulipa kisasi kwa mambo uliyofanyiwa ambayo hayakupendezi. Ikiwa ni masuala ya kikabila, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kidini, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kifamilia, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kikazi, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya uhusiano wako na majirani zako, usilipe kisasi.Ndiyo! Usilipe kisasi! Kwa nini? Kwa sababu "imeandikwa kisasi ni juu yangu Mimi; Mimi nitalipa, anena Bwana".

Lakini ikiwa utaona ya kuwa Mungu hawezi kukusaidia na ukaamua kujichukulia madaraka ya kujilipiza kisasi hasara zifuatazo hakika zitakupata!

Hasara ya Kwanza ya kulipiza kisasi

Lazima utashindwa hiyo vita!


Katika jambo lolote lile lililokukasirisha - liwe la kidini, au kikabila, au kifamilia, au kikazi, na kadhalika ukiamua kulipa kisasi utashindwa wewe kwa sababu vita hivyo si vya mwili na wala silaha ambazo Mungu amekupa si za mwili! imeandikwa
Tena katika kitabu cha Waefeso 6:12 imeandikwa hivi: "Kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho".

Uwanja wa mapambano Ulio mbele yako ni "ulimwengu wa roho" na mapambano uliyo nayo "si juu ya damu na nyama" - ingawa unaona ya kuwa ni watu na ni binadamu kama wewe wanaokusonga  wanatumiwa tu na ibilisi!
imeandikwa hivi 2 Wakorintho 10:3- 5:"Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi yamwili; maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome, tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo".

 Imeandikwa katika kitabu cha Ayubu 1:12-21 shetani anaongea na Mungu ila wanaokwenda kwa ayubu ni waseba,

Mbinu mojawapo mapepo yanayotumia kukutesa  ni kukufanyia kitu kitakachokukasirisha ili uamue kujibu au kushindana kimwili,kushambulia, kwa sababu anajua ukishindana "kimwili" au katika mwili utashindwa hakika, maana vita hivyo si vya mwili wala silaha ambazo Mungu amekupa si za mwili! Kwa sababu vita ni vya bwana,
 Warumi 8:31 Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?

Hasara ya Pili ya kulipiza kisasi

JIANDAE KUISHI NA MATATIZO HAYATAKWISHA!


Ikiwa umeamua kulipa kisasi kwa kumfanyia ubaya yule aliyekufanyia - ubaya hautakwisha, kwa sababu utavuna ulichopanda.Ndiyo maana imeandikwa hivi:"Yeye arudishaye mabaya badala ya mema, mabaya
hayataondoka nyumbani mwake" (Mithali 17:13)
Kumbuka imeandikwa hivi katika kitabu cha Wagalatia 6:7; "Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote ampandacho mtu. Ndicho atakachovuna"

kisasi katika ndoa
Ukiamua kulipiza kisasi kwa kumfanyia ubaya yule wa nyumbani mwako  Neno la Mungu inasema "mabaya hayataondoka nyumbani mwako" Hii ndiyo maana matatizo mengi katika ndoa na katika jamii hayaishi - kwa sababu mtu akifanyiwa ubaya naye analipa kisasi. Ubaya unaendelea kudumu,

kisasi na wenye mamlaka mabaya hayataondoka
Ukiamua kulipa kisasi kwa kumfanyia ubaya yule wa kazini kwako - fahamu mabaya hayataondoka kazini kwako. Ikiwa ni shuleni - mabaya hayataondoka hapo shuleni.

Tena hali ya mwisho inakuwa mbaya zaidi,kila wakati kisasi kinapoendelea kupandwa. Kwa sababu ukiwapa watu ubaya - nawe utapewa ubaya kwa; "kipimo cha kujaa na kushidiliwa, na kusukwa - sukwa - hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile upimacho ndicho mtakachopimiwa (Luka 6:38)

Kumbuka huwezi kuushinda ubaya  kwa ubaya mwingine, bali unashinda kwa wema - kama vile dawa ya chuki si chuki bali upendo! Ndiyo maana Warumi 12:21 inasema; "Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema".

Hasara ya Tatu:

UNAMZUIA MUNGU KUKUPIGANIA


Unaweza ukashangaa, lakini ndivyo ilivyo! Ukiamua kulipa kisasi juu ya tatizo ulilonalo - unamzuia Mungu asikusaidie kulitatua.Mungu hawezi kukusaidia kwa sababu imeandikwa "msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana, imeandikwa, kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana".

Neno "ipisheni" limeandikwa kwa sababu kulipa kisasi "kunazuia" ghadhabu ya Mungu isipigane upande wako! Tena si hivyo tu lakini ukilipa kisasi unaingilia kazi ambayo si yako! Ni kazi ya Mungu maana

Hatua yako ya kulipa kisasi inazuia mkono wa Mungu kukupigania - kwa hiyo ipishe ghadhabu ya Mungu kwa kutokujilipizia kisasi!

Hasara na Nne ya kulipiza kisasi,

katika ulimwengu wa roho wewe ni Muuwaji!


Unapoamua kulipa kisasi, unajichumia dhambi! Hii ni kwa sababu kulipa kisasi huja kwa njia ya chuki iliyojengeka ndani yako kwa ajili ya mambo mabaya uliyofanyiwa. Huwezi kulipa kisasi bila ya kumchukia huyo unayejilipizia kisasi kwake. Na imeandikwa

"Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajuaya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake" (1 Yohana 3:15).

Umeona hilo! Chuki huzaa kisasi, na huzaa dhambi ya kuua! Na

Hasara na Nne ya kulipiza kisasi,
Unaficha uso wa Mungu bila ya wewe kujuwa yaani maombi yako hayafiki popote na unapopita katika hali ngumu unakuwa peke yako Isaya 59:2b inasema; "dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia". Wale vijana watatu walipita katika moto wakiwa na Mungu

Kwa hiyo kama umekwisha lipa kisasi au umekusudia moyoni mwako kulipa kisasi kwa mtu yeyote aliyekutenda lolote, ni muhimu kufaham kuwa unakaribisha msiba, wa maisha,kazi,ndoa,uchuma,biashara, 
utubu ili Mungu akusamehe na mawasiliano yako na Yeye yawe mazuri. Mathayo 6:9

Hakuna kitukinachomfurahisha adui yako Kama anapogunduwa kuwa wewe huna ufahamu wowote juu ya uwezo alio nao hakuna jeshi duniani linalokubali silaha zake zote zijulikane, kwasababu silaha ni nguvu ni uwezo kwa aliye nayo kama ilivyo mtu mwenye maarifa huyo mtu ana nguvu, uwezo wa kufanya anachotaka kufanya,
Kila mwanadamu hapa duniani anafanya sawa sawa na ufahamu wake aliyo nao kwa lugha nyepesi kila unalolifanya unafanya kwa wingi na ukubwa wa taarifa ulizonazo juu ya kile unachokifanya, huwezi kufanya Zaidi ya kile unachokifahamu,
Imeandikwa katika wakolosai 3:16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
Ibilisi yake yeye ni kuuwa, yohana 10:10